Waziri Ummy apiga marufuku kuchangisha fedha ujenzi wa madarasa yaliyotengewa fungu la UVIKO-19

NA ANGELA MSIMBIRA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.Ummy Mwalimu amepiga marufuku wananchi kuachangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa yanayojengwa na fedha zilizotolewa kwa ajili ya UVIKO-19.
Ametoa agizo hilo Novemba 23,2021 wakati akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.

Ameendelea kufafanua kuwa  Serikali haikatazi wananchi kuchangia nguvu kazi kwa kuwa wamekuwa wakijitoa katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Seikali katika kuleta maendeleo.

Amesema kuwa, ujenzi wa madarasa kwa fedha za UVIKO-19 19 zimeletwa za kutosha na zinajitosheleza hadi kukamilika kwa ujenzi huo, hivyo wananchi wasilazimishwe kuchangia fedha za ujenzi huo.
Waziri Ummy amesema kuwa, anashangazwa na maelezo ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ya kuwatoza wananchi shilingi 5000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa hayo.

"Fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya kidato cha kwanza zinajitosheleza hadi ukamilishaji wake, inanishangaza ninyi mnawataka wananchi wachangie, naagiza ni marufuku kwa wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi,"amesema Waziri Ummy.

Ameendelea kusema kuwa, wananchi wanatakiwa kuchangia nguvu kazi kwa kusaidia kuchimba msingi, kubeba mawe, kuchota maji, kusogeza mchanga na kubeba matofali na sio kutozwa fedha.
Aidha, uchangiaji wa mwananchi si lazima bali ni hiari na pia wananchi kwa hiari yao wanaweza kuchangia vifaa vya ujenzi kadri watakavyoona inafaa, lakini sio kulazimishwa kuchangishwa pesa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news