Yanga SC yatembeza kipigo, Azam FC yajibebea dhahabu bure

NA GODFREY NNKO

Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hatua ambayo inaendelea kuwaweka katika mstari mzuri.
Chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi, Wanajangwani wamezitumia dakika tisini kuachia kipigo cha mabao matatu kwa moja kwa Ruvu Shooting katika mtanange wa Novemba 2, 2021 uliopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Dakika 45 za kwanza zilianza kwa kasi na nguvu kubwa baada ya timu zote mbili kulazimisha sare ya 1-1.

Ruvu Shooting walienda mapumziko huku wakiwa na pengo baada ya nahodha wao Santos Mazengo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 24.

Bao la Ruvu Shooting limefungwa na Shaban Msala dakika ya 10, baada beki wa Yanga SC, Dickson Job kuugusa mpira na kumpoteza golikipa Djigui Diarra.

Kocha wa Ruvu Boniface Mkwasa alilazimika kufanya mabadiliko ya kumtoa Marcel Kaheza na kumuingiza beki Ally Mtoni ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi.

Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Sogne alipata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo huku nafasi yake ikichukuliwa na Saido Ntibanzonkiza.

Yanga iliendelea kulishambulia lango la Ruvu Shooting ambapo dakika ya 32, Feisal Salum (Fei Toto) aliipatia Yanga SC bao la kusawazisha baada ya kupiga shuti kali nje ya 18, lililomshinda golikipa Mohamed Makaka.

Kwa matokeo hayo, Yanga SC inafikisha alama 15 baada ya kushinda mechi zote tano tangu msimu uanze na kuendelea kuongoza ligi kwa alama tano zaidi ya Polisi Tanzania wanaofuatia wakati Ruvu Shooting inabaki na alama zake sita za mechi tano.

Wakati huo huo, Azam FC imetwaa alama zote tatu katika mtanange wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold FC.
Ni baada ya kuichapa Geita Gold FC bao 1-0 katika mtanange uliopigwa ndani ya dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Azam walipata bao lililowekwa nyavuni na Kola ndani ya dakika 81 kwa shuti akimalizia kazi nzuri ya krosi kutoka kwa Tepsie.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news