Bernard Morrison apewa tuzo, ikiwa ni mwendelezo wa furaha ya ushindi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WINGA Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, Bernard Morrison ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa klabu hiyo mwezi Novemba na kukabidhiwa kiasi cha shilingi milioni 2 kutoka kwa wadhamini ambao ni Kampuni ya Emirate Aluminium ACP.
Ushindi huo unakuja, baada ya awali waajiri wake ambao ni Simba SC kutembeza kichapo cha 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ni mtanange wa aina yake ambao ulipigwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.

Mmalawi Peter Banda dakika ya tisa na mzawa, Muzamil Yassin dakika ya 57 ndiyo walioharibu mipango ya Geita Gold huku wao Juma Mahadhi dakila ya 66 akiwapunguzia makali ya maumivu.

Simba SC imefikisha alama 17 ingawa inabaki na nafasi ya pili ikizidiwa alama mbili na Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi saba kuelekea mechi baina yao Desemba 11,2021 katika dimba hilo.

Post a Comment

0 Comments