CCM yampongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kuwarejeshea fedha waliokuwa wanaidai Kampuni ya Masterlife

NA MWANDISHI MAALUM

KIKAO cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimetoa azimio la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa maamuzi yake ya kuwarejeshea fedha zao wananchi waliokuwa wanaidai Kampuni ya Masterlife.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kilichofanyia Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, mjini Zanzibar leo. Katikati ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.

Kampuni ya Masterlife Microfinance Ltd ambayo inadaiwa ilikuwa ikiendesha shughuli za kifedha Zanzibar kinyume na sheria na taratibu za nchi, ilikusanya fedha nyingi kutoka kwa wananchi 11,000.

Desemba 7, 2021 Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar ilianza kuwalipa waoweka fedha katika kampuni hiyo awamu ya kwanza ambao wanadai kati ya shilingi 100, 000 hadi shilingi milioni moja.
Wajumbe wakiwa wamesimama wakati Dkt.Shein akiingia ukumbini kuongoza kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein baada ya kuigia ukumbini. Katikati ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Pia kikao hicho kimempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani, na kuridhishwa na uongozi wake wenye mafanikio makubwa yakiwemo kudumisha hali ya amani, utulivu na mshikamano kwa wananchi wote.

Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Zanzibar.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dkt.Abdallah Mabodi alipokuwa akifungua kikao hicho.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa mbalimbali za kiutendaji kutoka katika idara za CCM Zanzibar na pia kumepokea na kujadili taarifa ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dkt. Mwinyi aliyoifanya katika mikoa sita ya CCM Kichama.

Kikao hicho ni cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977, Toleo jipya la mwaka 2017, Ibara ya 108 (2), inayofafanua kwamba Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja kila miezi mitatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news