Kamilisheni Kituo cha Afya Nata tulete vifaa tiba-Waziri Ummy

NA NTEGHENJWA HOSSEAH,OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu amekagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Nata kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora na kuahidi kuletea vifaa tiba mara Kituo hicho kitakapokamilika.
Akiwa kituoni hapo amewaelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa Kituo hicho cha Afya kwa wakati na Ofisi ya Rais TAMISEMI wataleta vifaa tiba na vitendanishi vyenye thamani ya shilingi Mil 500.

Akitoa Taarifa ya Kituo hicho Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa kituo hicho Bw. Katunzi Jackson Kihembe amesema majengo yanayojengwa katika kituo hicho ni jengo la Wazazi, Upasuaji, Maabara na Jengo la wagonjwa wa nje. 

Kituo cha Afya Nata kinategemewa kukamila January,2022 na kitatoa huduma kwa wakazi wa kazi ya Nata wapato 19,873.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news