KMC FC ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar leo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KIKOSI cha KMC FC leo kitashuka katika uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa saa 16:00 jioni.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC, Christina Mwagala.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ambayo iliwasili mkoani hapa awali ikitokea jijini Dar es Salaam imefanya maandalizi yake ya mwisho jana kabla ya mchezo na kwamba kikosi hicho cha wana Kino Boys kipo tayari kwa mtanange huo muhimu.

KMC FC ambao watakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar inahitaji kufanya vizuri katika mchezo huo ili kuendelea kujiimarisha zaidi katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC licha ya kuwa inakwenda kukutana na timu yenye ushindani lakini KMC ni bora zaidi na kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa.

KMC FC ambayo ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara imejiandaa vema kupata matokeo mazuri ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kuwa kama Timu inapata ushindi kwenye michezo yake yote licha ya kuwepo kwa ushindani mkubwa kwa Timu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu.

“Ukiangalia kwenye msimamo wa Ligi bado kunaushindani mkubwa, kila Timu inahitaji kupata matokeo mazuri, lakini KMC tunahitaji ushindi mzuri kwa umuhimu wa namna yake, tunafahamu kuwa utakuwa mchezo mgumu, lakini sisi tunakwenda uwanjani kupambania alama tatu muhimu,"amesema.

"Ukiangalia wapinzani wetu kwenye michezo yao wamefanya vizuri, lakini haifanyi sisi tukakosa matokeo, kwa sababu kila mmoja amejipanga kwa namna yake, kikubwa tunamuomba mwenyezi Mungu atupe uzima,"ameongeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news