Kocha Thierry Hitimana aondolewa Simba SC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UONGOZI wa Simba SC umeachana na kocha wao, Mnyarwanda Thierry Hitimana baada ya miezi mitatu ya ajira.
Kocha Hitimana alitambulishwa kama kocha Msaidizi Simba Septemba 11 na baada ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa kujiuzulu Oktoba 26, Mnyarwanda huyo akakaimu nafasi ya Kocha Mkuu. 

Kocha huyo ambaye ana leseni ya CAF daraja A awali safari yake ilikuwa ni kurudi Mtibwa Sugar aliyokuwa amewahi kuitumikia katikati ya msimu kisha kung'atuka kwa madai ya kutoelewana na wasaidizi wake kwenye benchi la ufundi.

Post a Comment

0 Comments