🔴 LIVE: Rais Samia katika Hafla ya Utiaji Saini Mikataba Baina ya Serikali na Kampuni za Uchimbaji Madini ukumbi wa JNICC

LEO Desemba 13, 2021 inafanyika Hafla ya Utiaji Saini Mikataba Baina ya Serikali na Kampuni za Uchimbaji Madini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Uwekaji Saini ya Makubaliano unafanyika kati ya Serikali na Kampuni za Uchimbaji Madini za Black Rock Mining Limited, Strandline Resources Limited na Nyanzaga.

Post a Comment

0 Comments