Mahafali ya TIA yafana, wahitimu waaswa kuzingatia weledi

>Dkt.Momole ataja mafanikio ya taasisi kwa wahitimu wenye ushindani wa soko la ajira

NA MWANDISHI MAALUM

MHASIBU Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Leonard Mkude amewataka wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kujiendeleza kielimu ndani ya ajira ili kwenda na kasi ya ukuaji katika kufanya kazi kwa weledi na ubunifu ili kuiletea nchi maendeleo.
Baadhi wahadhiri na watendaji wa TIA katika mahafali ya 19 yaliyofanyika Kampasi ya Dar es Salaam.
Mgeni rasmi pamoja na meza yake wakiwa katika heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kufunguliwa kwa mahafali ya 19 ya TIA.
Akizungumza Desemba 3,2021 kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo katika mahafali ya 19 ya chuo hicho, Mhasibu Mkuu amesema wanafunzi hao hawapaswi kubweteka na elimu waliyoipata, wanatakiwa kutambua kuwa wanakwenda kuwatumikia wananchi pamoja katika sekita mbalimbali nchini hivyo ni wajibu wao kutanguliza weledi wa kazi ikiwa ni pamoja na kujiepusha na rushwa.
Baadhi ya picha za wahitimu wakiwa wamesimama katika mahafali ya 19 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika katika Kampasi ya Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya wahitimu zaidi ya 7000 kwa kampasi mbili amesema, “ninawaasa wanafunzi mnaohitimu ngazi mbalimbali kutambua kwamba elimu mnayoipata iwe chachu ya kujiongezea maarifa. Msiwe wataalamu wasio na tija katika kuleta maendeleo.”
Amewataka kutumia elimu waliyoipata kujitafutia soko la ajira na kujiajiri pamoja na kuwa wabunifu kutokana na ushindani wa soko la ajira.
Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango,Leonard Mkude akizungumza wakati wa kufungua mahafali ya 19 ya Taasisi ya Uhasibu Tananzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika Kampasi ya jijini Dar es Salaam.

“Soko lililopo la ajira ni dogo, ni vyema mkaelekeza mawazo yenu kwenye kujiajiri na si kuajiriwa,"amesema.

Mkude amesema, Watakaobahatika kuajiriwa wajitahidini kufanya kazi kwa bidii na ubunifu na kujiepusha na rushwa kwani inashusha taaluma ambazo wamepata katika chuo hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Wakili Said Chiguma akizungumza katika mahafali hayo.

“Mmetoka hapa kwa kuandaliwa kama wataalam, hivyo msiache kuitumia elimu hiyo katika kuleta maendeleo ya nchi na kuwa bora zaidi katika soko la ajira,"amesema.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt. Momole Kasambala akizungumza kuhusiana na mahafali ya 19 ya taasisi hiyo yaliyofanyika Kampasi ya Dar es Salaam.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt.Momole Kasambala amesema, zaidi ya wahitimu 7000 ambao wametunikiwa taaluma ambapo chuo kimekuwa na mafanikio na kufanya kila nwaka kuongeza udahili wa kujiunga.

Dkt.Kasambala amesema kuwa, licha ya mafanikio hayo lakini Chuo kimejiimarisha katika kuhakikisha wahitinu wanakwenda kuwa mabalozi wa taasisi.

Dkt. Momole amesema, TIA itaendelea kuhuhisha mitaala inayoendana na mahitaji ya kitaifa na kimataifa kama dira ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania inavyosema “Kuwa Taasisi inayotoa elimu yenye ubora katika biashara, huduma za utafiti na Ushauri barani Afrika.

“Nawapongeza Wahitimu wote mkalitumikie Taifa letu kwa tija na uzalendo,” alisisitiza.

Post a Comment

0 Comments