Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya juu Tanzania afanya uteuzi na kutengua katika kamisheni mbalimbali

NA GODFREY NNKO

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO),Ndg. FRANK NKINDA amefanya uteuzi na mabadiliko katika Kamisheni mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Ofisi ya Mwenyekiti TAHLISO, Janet O. Gasarasi mabadiliko na uteuzi huo umefanyika Novemba 30,2021.

Katika uteuzi huo, Mwenyekiti amemteuwa Ndg. EMMANUEL MARTIN kuwa KAMISHNA WA MIKOPO.

Emmanuel Martin alikuwa Naibu Kamishna wa mikopo hapo awali, Naibu Kamishna wake atakuwa, Ndg. FRED ROMANAS SANGA ambaye ni Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu. Nyerere- Magogoni jijini Dar es Salaam.

Pia Mwenyekiti amemteuwa, Ndg. AMANI MDEKHA kuwa KAMISHNA WA MIPANGO NA FEDHA. Mdekha ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST) jijini Mbeya.

Aidha, amemteuwa, Ndg. FARIS BURHAN kuwa NAIBU KAMISHNA - MAKONGAMANO NA MIDAHALO.

Faris ni Mwanafunzi wa Masters Chuo Kikuu Dodoma, Kamisheni hii itakuwa na Manaibu wawili na itaboreshwa kulingana na mazingira na wakati.

Sambamba na uteuzi huo, Mwenyekiti huyo ametengua uteuzi wa Kamishna na Naibu Kamishna wa Jinsia na Maendeleo ya Wanawake Vyuoni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa viongozi wa Kamisheni hih utafanywa hapo baadae.

"Uteuzi wa Kamishna umeanza hii leo Novemba 30,2021) na wote walioteuliwa wataapishwa tarehe 4, Desemba,2021 Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa TAHLISO,"imeongeza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news