Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Mustapha Semwaiko Yussuf kupitia barua yenye kumbukumbu Na. KDC/L.50/9VOL.1/123 amewatamgazia waombaji wa nafasi za kazi ya utendaji wa Kijiji Daraja la III na Katibu Muhtasi Daraja la III waliokidhi vigezo kufika kwenye usaili.

Usaili huo utafanyika katika Ukumbi wa Kondoa Irangi uliopo Kondoa Mjini Desemba 7, 2021 na Desemba 8, 2021 usaili wa ana kwa ana utafanyika makao makuu ya halmashauri (Bukulu) kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa maelekezo ya Mkurugenzi huyo, waombaji waliokidhi vigezo kama orodha inavyoonesha hapa chini wafike na vyeti halishi (original) vifuatavyo; mosi cheti cha kuhitimu kidato cha nne, pili cheti cha taaluma ngazi ya astashahada (certificate-NTA LEVEL 5), tatu kitambulisho cha Taifa, kitambulisho cha mpiga kura, leseni ya udereva au hati ya kusafiria kwa ajili ya utambulizi, nne cheti cha kuzaliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa amebainisha kuwa, waombaji ambao majina yao hayajaonekana katika orodha, watambue kuwa hawajakidhi vigezo stahiki.

Pia amewataka waombaji kutambua kuwa, gharama za kuhudhuria usaili kila mmoja atajigharamia mwenyewe kwani halmashauri haitahusika.

Post a Comment

0 Comments