Rais Dkt.Mwinyi atoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kwa kula kasa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kufuatia kula samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu huko Matemwe, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzinasihi familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hichi kigumu cha msiba pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwaponya kwa haraka waliodhurika baada ya kula samaki huyo.

Rais Dkt. Mwinyi katika salamu hizo za rambirambi, amesema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake husika itaendelea kuhakikisha wale wote waliodhurika wanaendelea kupatiwa tiba ili waweze kurudi katika hali zao nzuri za kiafya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news