Rais Maduro aitaka jumuiya ya Kimataifa kulaani mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani mwaka 2020

CARACAS-Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Venezuela, Mheshimiwa Nicholas Maduro amesema, jamii ya Kimataifa inapaswa kulaani vikali mauaji ya kigaidi ya mwaka 2020 ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akitoa hotuba yake baada ya kuapishwa kwa kipindi cha pili mjini Caracas nchini humo Januari 10, 2009. Licha ya vikwazo vingi ambavyo utawala wake umekuwa ukipitia amekuwa akisimama imara kuhakikisha anakitimiza kile anachoamini kwa maslahi ya wananchi na Taifa lake. (Picha na Yuri Cortez—AFP/Getty Images).

Kiongozi ambaye wakati wa uhai wake alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi ndani na njew ya jamhuri hiyo.

Rais Maduro ameyasema hayo katika mahojiano na runinga ya Al Mayadeen ya Lebanon ambapo amelaani mauaji ya Soleimani yaliyofanywa na Marekani na kuyataja kuwa ni jinai ya kuogofya na isiyokubalika.

"Je? Hii ndio Dunia tunayoitaka, ambayo Ikulu ya White House inatoa amri ya kuuawa shujaa wa vita dhidi ya ugaidi Iraq, Syria na Lebanon? Inasikitisha sana. Jenerali Soleimani alikuwa mwenye tabasamu na matumaini. Namshukuru Mungu kwa kukutana naye," Rais Maduro amesema hayo akiwa anakumbuka namna Luteni Jenerali Soleimani alivyotembelea Caracas kati ya Machi na Aprili mwaka 2019. 

Rais Maduro amesema,Luteni Jenerali Soleimani alipambana na magaidi na watenda jinai ambao walikuwa wakiwashambulia raia wa kawaida na mhimili huku akiszisitiza kuwa alikuwa ni shujaa wa kipekee.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye Januari 3, mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane.

Ni katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad ambapo inaelezwa hujuma hiyo ilitekelezwa kufuatia amri ya rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump. 

Rais wa Venezuela pia amesema uhusiano wa nchi yake na Iran ni mzuri na kuongeza kuwa atafika Tehran hivi karibuni kufuatia mwaliko wa Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news