Rais Samia afanya uteuzi leo Desemba 2,2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Salome Thaddaus Sijaona kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Sijaona anachukua nafasi ya Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu ambaye amemaliza muda wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jafar Haniu, uteuzi huo umeanza leo Desemba 2, 2021.

Post a Comment

0 Comments