Rais Samia kuzindua kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za radi

NA ROTARY HAULE

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara leo katika Wilaya ya Mkuranga iliyopo mkoani Pwani kwa ajili ya kuzindua kiwanda cha kutengenezea nyanya za radi kinachojulikana kwa jina la Raddi Fibre Manufacturing Limited.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewaeleza waandishi wa habari Desemba 2,2021 ofisini kwake kuwa kufanyika kwa ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru itakayofanyika Desemba 9, mwaka huu.

Kunenge amesema kuwa, mkoa umepata heshima kubwa ya kutembelewa na Rais hasa katika kuzindua kiwanda hicho kikubwa ambacho kinashika nafasi ya nne barani Afrika.

Amesema,kiwanda hicho kinatanguliwa na kile kilichopo Misri,Algeria,Afrika Kusini na Tanzania ambapo kinachangia uchumi mkubwa wa wilaya,mkoa na Taifa kiujumla.

"Tunatarajia kupokea ugeni wa Rais wetu Samia katika Wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya kuzindua kiwanda kikubwa cha radi, nyaya za kutengenezea mkondo wa mawasiliano ambacho kinashika nafasi ya nne barani Afrika ,"amesema Kunenge.

Kunenge ameongeza kuwa, kiwanda hicho pia kinaipa heshima Afrika Mashariki na Kati na hiyo ni sera ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia katika kukuza masuala ya uwekezaji katika viwanda.

Aidha, Kunenge amemshukuru Rais Samia kwa kufanya ziara hiyo Mkoani Pwani licha ya kuwa na ratiba nyingi za kutekeleza majukumu kwa ajili ya Watanzania na kwamba lazima aungwe mkono.

Amesema,kabla ya Rais kufika kiwandani hapo atasalimiana na wananchi wa Vikindu ambapo amewaomba wananchi waliopo katika maeneo hayo wajitokeze kwa ajili ya kumlaki Rais.
Kunenge amesema akiwa kiwandani hapo atakagua kiwanda hicho na kufanya uzinduzi ambapo amewaomba pia wananchi waliopo katika Wilaya ya Mkuranga pamoja na viongozi wote kujitokeza kwa wingi katika kushuhudia uzinduzi huo.

"Mimi naomba wananchi wa Mkoa wa Pwani wajitokeze kumpa sapoti Rais wetu anapokuja Wilaya ya Mkuranga maana ametupa heshima kubwa wana Pwani, kwa hiyo lazima tuitumie vizuri nafasi kwa kuwepo kwa wingi eneo la tukio,"amesema Kunenge.

Amesema, uzinduzi wa kiwanda hicho ni muendelezo wa kupanua wigo wa kiuchumi kupitia viwanda na mkoa tayari umejipanga kuhusu kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji wa viwanda.

Amewataka wawekezaji kuendelea kujitokeza mkoani Pwani kwa ajili ya uwekezaji kwa kuwa fursa zipo na bado zinahitaji wawekezaji na kwamba yeyote anayetaka kuwekeza Pwani ajitokeze kupitia utaratibu maalum..

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news