Ruvu Darajani yaichapa Meena FC 2-0

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TIMU ya soka ya Ruvu Darajani imeichapa timu ya Meena Fc kwa magoli 2-0 kwenye mashindano ya Meena Cup ambapo mshindi atajinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja taslimu na mipira miwili.
Kwenye mchezo huo wa ufunguzi wa ligi hiyo mchezo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mtongani Mlandizi Kibaha Darajani walipata magoli yake kupitia kwa Erasto Mwingereza na Ibara Mbegeze.

Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 12 itaendelea leo kwa mchezo baina ya Super Academy na Wapolo Fc kwenye uwanja huo huo wa Shule ya Msingi Mtongani. 

Akizungumzia juu ya mashindano hayo ya Meena Cup mratibu wa mashindano hayo Hubert Kingu alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuinua vipaji vya soka na kuhamasisha vijana kujiunga na Shule ya Victory Academy ambapo mbali ya kutoa elimu ya kawaida kwa shule awali na msingi pia inasehemu ya michezo.

Kingu alisema kuwa pia timu ya Meena nayo inashiriki mashindano hayo inatokana na shule hiyo ya Victory ambapo vijana wanafundishwa mpira.

"Kuhusu zawadi mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na mipira miwili, mshindi wa pili atajinyakulia 500,000 na Mpira mmoja," alisema Kingu.

Alisema pia kutakuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo kwa mchezaji bora, kipa bora, mfungaji bora, mwamuzi na kikundi bora cha ushangiliaji ambapo kila mmoja atajinyakulia 50,000.

Aidha alizitaja timu zitakazochuana kuwa ni pamoja na Ruvu Darajani, Meena B, Super Academy, Vancouver Fc, Miswe Fc kutoka kundi A.

Timu za kundi B ni Visiga Morning, Mlandizi Stars, Mtongani Fc, Meena Fc, Pita na zako Fc na Mlandizi Kids.

Post a Comment

0 Comments