Serikali yatoa Bilioni 2.3/- Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori (Mweka)

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI imefanikiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa bweni katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyanyamapori (Mweka) kilichopo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kutoa shilingi bilioni 2.46 kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.
Profesa Jafari Kideghesho ambaye ni Mkuu wa chuo hicho ameyasema hayo kwenye mahafali ya 57 chuoni hapo.

Amesema, kuwepo kwa bweni hilo kutapunguza changamoto ya uhaba wa malazi kwa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kuongeza usalama na udhibiti nidhamu kwa wanafunzi chuo hapo.

Professa Kideghesho amesema, bweni hilo lina uwezo wa kulaza wanafunzi 295 na mradi wa ujenzi wa bweni hilo umetekelezwa na mkandarasi SUMA JKT, ambapo mradi huo ulianza Mei 25,2020 ambao kwa sasa umefikia asilimia 99.

"Kati ya vyumba vilivyomo katika bweni hili, vyumba 15 ni vyumba maalumu (VIP), vyumba 70 ni vyumba vya kawaida na kila sakafu ina chumba cha kupumzikia, maliwato na sehemu za kufanyia usafi wa nguo, jengo hili lina uwezo wa kuwahudumia wanafunzi wapatao 295,"amesema.

Amesema, mradi huo wa ujenzi wa hosteli hiyo ya wanafunzi umetekelezwa na mkandarasi SUMA JKT ambaye alihusika kufanya kazi za usanifu wa ramani za ujenzi, utekelezaji na ujenzi huo umechukua miezi 18 hadi kukamilika kwake.

"Hosteli hii itapunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la uhaba wa malazi kwa wanafunzi na kuongeza usalama na udhibiti wa nidhamu kwa wanafunzi wetu chuoni hapa,"amesema Prof. Kideghesho.

Awali akizindua hosteli hiyo, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephan Kagaigai, aliwataka wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo hicho kuhakikisha kwamba wanaitunza miundombinu hiyo vizuri ili iweze kuwasaidia kwa kipindi kirefu.

"Niwaombe menejimenti ya chuo kupata jengo zuri kama hili ni jambo moja, changamoto inayokuwepo ni namna ya kulitunza, namna ya usimamizi, humu watakuwa wanaishi binadamu, binadamu ambao mtakuwa mnawapata, nimeambiwa watakuwa wakitoka mataifa mbalimbali na maeneo mbalimbali, ni watu wenye malezi tofauti tofauti, kwa hiyo mkuu wa chuo pamoja na bodi yako ni namna ya kusimamia hili jengo, ili miundombinu yake iweze kuwa endelevu,"amesema..

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news