Shirika la Ecan (T) waja na mkakati kukabiliana na Ukatili Kiteto

NA MOHAMED HAMAD

KUTOKANA na kukithiri vitendo vya ukatili Wlwilayani Kiteto mkoani Manyara, Shirika la Ecan (T) wilayani humo limeanza mikakati ya kukabiliana na vitendo hivyo.
Samwel Maphie mratibu wa Shirika la Ecan (T) akiwa kwenye mjadala na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mtakuwa wakijadiliana.

Mkakati huo ni kutoa elimu kwa kamati za Mtakuwa maeneo ya mradi wa shirika hilo Kata za Kibaya, Kaloleni, Bwagamoyo na Bwawani.

Mratibu wa shirika hilo, Samwel Maphie, alitaja aina za ukatili Kiteto kuwa ni vipigo kwa akina mama, mimba za utotoni kwa wanafunzi shuleni na ukatili wa kingono kwa wanandoa.

Shirika kwa kuona ukubwa wa tatizo hilo limeanza kupunguza ukatili kata nne, kutoa elimu ya madhara ya ukatili ambapo watawafikia viongozi wa Dini, Mila, na watu maarifu kupitia Kamati za Mtakuwa za vijiji na Kata.

Akizungumzia Ukatili huo Mzee Mwinyi Mwinyimvua, Mzee maarufu alisema kwa sasa elimu zaidi inahitajika ndani ya jamii na kudai madhara makubwa yanazidi kijitokeza vikiwemo vifo.

"Ukitaka kuona ukatili ni mkubwa Kiteto angalia jinsi watoto walivyokatishwa masomo kwa kupachikwa mimba na wengi wao wamezaa watoto pamoja na kwamba ukitaka kuwapata wahalifu huwapati kwani wanafichwa,"amesema.

Amesema, kesi nyingi zimefutwa mahakamani na watoto wenyewe waliopachikwa mimba ndio wanaharibu kesi zao kwa kutowataja wahusika ili wasitiwe hatiani.
Elias Mwinuka mwanasaikolojia akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Mtakuwa Kiteto.

Mwanasaikolojia Elias Mwinuka, alitaja chanzo cha madhara hayo kuwa ni matokeo ya baadhi ya wazazi na walezi kutotimiza wajibu na majukumu yao ya kulea watoto huku wakitupia lawama Serikali kuwa maisha ni magumu.

Alisema mtoto ana walinzi wengi wakiwemo wazazi na walezi, Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali ambao kwa pamoja wamekuwa wakifanya kazi ya kumlinda mtoto lakini bado watoto wanafanyiwa ukatili kila kukicha.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Polisi Kiteto, Aisha Salehe akiongea na kundi maalumu la wasicha waliokatishwa masomo yao kwa kupachikwa mimba.

Afisa Ustawi wa Jamii Kiteto, Jackline Barongo alisema Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali wamekuwa na jitihada kukabiliana na vitendo vya ukatili lakini baadhi ya jamii wamekuwa wakiwaficha wahalifu na hata kuwahadaa watoto wanaopachikwa mimba kusema uongo mahakamani.
Rodrick Kidenya akiongea na Young Mothers katika moja ya kikao kikichoandaliwa na Shirika la Ecan (T) mjini Kibaya.

Afisa maendeleo ya Jamii Kiteto, Rodrick Kidenya katika sakata hilo alisema Mashirika yamekuwa msaada mkubwa katika kuisaidia Serikali na kuomba kuongeza jitihada.

Naye Bakari Mdillah Katibu wa Bakwata Wilaya ya Kiteto alisema ukatili upo ndani ya jamii na kuomba Serikali kusimamia sheria kwani hakuna asiyefahamu madhara ya ukatili.

Post a Comment

0 Comments