Simba Queens watembeza dozi Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MABINGWA watetezi, Simba Queens wameendelea kugawa dozi kwa wapinzani katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya kuichapa Oyster-bay Girls 8-0 jioni ya leo Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Aisha Djafar matatu, Opa Clement na Aisha Mnunka kila mmoja mawili, wakati la nane Oysterbay Girls walijifunga. 

Kwa upande wa watani wao, Yanga Princess wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Fountain Gate Princess Uwanja wa Fountain Gate, Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments