TAMISEMI kutoa bilioni sita kujenga nyumba za watumishi wa elimu na afya nchini

NA NTEGHENJWA HOSSEAH-OR TAMISEMI

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inatarajia kutumia shilingi bilioni sita kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi wa afya na elimu katika halmashauri za vijijini.
"Kati ya vitu vinavyoniumiza kichwa ni kuona wimbi la watumishi wakitaka kuhama kutoka vijijini kwenda mjini.

"Nitakuwa Waziri wa hovyo kama nitaendelea kuruhusu uhamisho wa aina hii kwa sababu na kule vijijini kuna watoto ambao wanahitaji walimu wa kuwafundishia na wananchi wanaohitaji wataalamu wa afya wa kuwahudumia.

"Ndoa hazipo mjini tu hata wa vijijini wameoa na kuolewa, sasa kwa nini kila mtumishi anayemfuata mwenza anataka kuhamia mjini ina maana hakuna wenza walioko halmashauri za pembezoni;

Haya ni maneno ya mara kadhaa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mhe. Ummy Mwalimu anapokuwa kwenye ziara za kikazi katika mamlaka za Serikali za Mitaa na kuulizwa maswali kuhusu kusitisha kwa muda uhamisho wa watumishi.

“Nimefikiria mara nyingi namna gani naweza kuwamotivate (kuwapa motisha) watumishi wa Halmashauri za Vijijini ili waweze kufurahia mazingira yao ya kazi na kuacha kufikiria masuala ya kuhama na kwenda mjini,” amesema.

"Kati ya vitu vya mwanzo nilivyopanga ni kujenga nyumba za watumishi hao ili waweze kuishi kwenye mazingira bora yatakayowavutia kufanya kazi katika maeneo ya vijijini,"ameongeza.

Akiwa ziarani mkoani Tabora katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mapema leo amesema kuna, wakati mtu anapangiwa kazi kijijini kiasi kwamba hata nyumba ya kupanga ya maana hakuna, lakini tukijenga nyumba nzuri eneo hilo mtumisni huyo atakuwa na uhakika wa makazi bora.

"Katika kutekeleza hilo tutatoa bilioni sita na tumeelekeza fedha hizi zikajenga nyumba za watumishi 165 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,"amesema.

Akielezea nyumba hizo, Waziri Ummy amesema zitakuwa nyumba 54 za 3 in 1; yaani nyumba 1 itabeba familia 3 hivyo jumla itakuwa familia 162.

Amebainisha kuwa nyumba hizo zitajengwa kwenye Halmashauri za Wilaya na baadhi ya halmashauri za Mji ambazo hazina mapato makubwa; Halmashauri za Majiji na Manispaa hazitapata fedha hizo kwa kuwa wanaweza kutumia mapato ya ndani kujenga nyumba za watumishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news