Tanzania yakwama kushiriki Miss World 2021

NA MWANDISHI MAALUM

"Kesho Tarehe 3 December 2021 ndio mwisho wa kuingia kambi ya Miss World baada ya nchi nyingi kupata changamoto ya kuchelewa kupata Visa ya Marekani kwa wakati. Miss World wakaongeza muda na kuruhusu hadi ikifika hiyo kesho iwe mwisho.
Mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu yanafanyika nchini Puerto Rico , na Puerto Rico ni 'territory ' ya marekani hivyo utahitaji visa ya Puerto Rico moja kwa moja ama utahitaji kua na Visa ya Marekani hata kama hutaingia marekani ili kuweza kuingia Puerto Rico haswa kwa nchi za Africa, maana hamna Embassy wala consulate hata moja barani Africa.

Janga la Covid 19 nalo limebadilisha namna nzima ya upatikanaji wa Visa ya marekani appointment. Serikali ya Puerto Rico imejitahidi sana kuandika barua kwa ajili ya washiriki wote ikiwemo Miss Tanzania Organisation Juliana Rugumisa na kutuwezesha kupata appointment kabla ya January tatizo ni limi unaipata haijulikani kwa sababu ya system. ( mfumo) , hadi sasa passport ya Juliana bado iko ubalozini kusubiri Visa

Hii ndio kusema kwa mwaka huu haitawezekana tena. Hata hivyo mwisho wa mashindano ndio mwanzo wa mashindano yajayo. Tunashukuru sana partners wetu Miss World kwa jitihada kubwa na kuhakikisha hadi tunapata appointment mapema badala ya January , Serikali ya
Puerto rico ambao ndio wenyeji wamashindano , umoja wetu wa 'country coordinators ' dunia nzima imetufanya tumekua kitu kimoja badala ya kua washindani.

Mwaka huu tulikua na mwakilishi bora sana Juliana Rugumisa aliyetikisa dunia huu ni mwanzo na sio mwisho. Kwa mapenzi ya Mungu Miss World family tutakutana 2022.

Kwa mashabiki zetu msikate tamaa kwetu iwe muendelexo wa maandalizi kwa ajili 2022 ."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news