TRC yaongeza safari za treni Dar, Tanga, Kilimanjaro na Arusha

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa, kutokana na ongezeko la abiria wanaoelekea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha katika msimu huu wa Sikuu Kuu za Krisimasi na Mwaka Mpya limeongeza idadi ya safari.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo ambayo imefafanua kuwa, idadi ya safari kuanzia Desemba Mosi zitakuwa mara tatu kwa wiki.

"Ni kwa wiki katika siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kutoka Dar es Salaam na Jumanne, Alhamisi na Jumamosi kutoka Arusha,"imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Reli Tanzania, ili kukata tiketi unaweza kutembelea booking.trc.co.tz au kutembelea stesheni iliyopo karibu.

Post a Comment

0 Comments