Ujenzi wa daraja jipya la Simiyu wanukia

NA DENIZA CYPRIAN-WUU 

SERIKALI imesema ipo mbioni kuanza kumtafuta mkandarasi atayekejenga Daraja jipya la Simiyu lililopo katika barabara Kuu ya Mwanza – Musoma lenye urefu wa mita 139.92 na upana wa mita 3 ambalo limedumu takribani miaka 67 toka kujengwa kwake. 

Amesema hayo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, wakati akilikagua daraja hilo lililopo Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza na kuunganisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Arusha na nchi jirani ya Kenya na kusisitiza kuwa fedha tayari zimeshatengwa. 
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akikagua chini ya Daraja la Mto Simiyu lenye urefu wa mita 139.92 linalotarajiwa kujengwa upya na Serikali hivi karibuni. (PICHA NA WUU).

“Serikali imeamua kujenga Daraja hili lililojengwa toka mwaka 1954 ambapo sasa limechoka na hivyo Serikali imeitengea bajeti kwa mwaka huu wa fedha 2021/22 na kazi inayofata ni kuitangaza kupata mkandarasi na kulijenga upya na la kisasa,”amesema Prof. Mbarawa.
Muonekano wa Daraja la Mto Simiyu lililopo katika barabara kuu ya Mwanza – Musoma lenye urefu wa mita 139.92 ambapo Serikali imeamua kutenga fedha na kulijenga upya hivi karibuni. 

Prof. Mbarawa, amewatoa hofu wananchi wote wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani ambao wanatumia daraja hilo kusafirisha abiria na mazao sasa kilio chao kimesikika na daraja linaenda kujengwa na fedha zipo. 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli, amemueleza Waziri huyo umuhimu wa daraja hilo kukamilika kujengwa mapema kwani lina watumiaji wengi ambao ni wakulima, wavuvi, wafanyabiashara wanaosafirisha mazao yao kutoka eneo moja hadi jingine.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli (mwenye shati la kitenge), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), wakati akikagua Daraja la Mto Simiyu ambalo Serikali inatarajia kuanza kumtafuta mkandarasi kwa ajili ya kujenga daraja jipya. 

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mwaza, Mhandisi Boniface Mkumbo, ameeleza kuwa Daraja hilo litajengwa kisasa na litakuwa na uwezo wa kuruhusu magari mawili kupishana na sehemu za watembea kwa miguu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news