Waisrael waahidi neema kwa Tanzania

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi amekutana na Uongozi wa Shirika la Save a Child’s Heart na Hospitali ya Wolfson Medical Centre nchini Israel.
Taasisi hizo mbili zimekuwa zikishirikiana na Tanzania katika kutoa mafunzo ya watalaamu katika ubingwa bobezi wa upasuaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto.

Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Save a Child’s Heart, Simon Fisher wamekubaliana mjini Telaviv nchini Israel, Desemba 2, 2021 kusaidia mafunzo ya Watanzania zaidi katika upasuaji wa moyo huku wakiimarisha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kujenga uwezo pia kwa watalaamu wengine zaidi katika Hospitali za Kanda hasa za Benjamin Mkapa, Bugando,KCMC na Bugando.
Aidha, Hospitali ya Wolfson ipo tayari kutoa utalaamu na mafunzo katika maeneo mengine kama saratani na magonjwa ya tumbo.

Prof.Makubi ameuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ina nia ya dhati ya kuimarisha haya ushirikiano na kuboresha huduma za afya nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news