WAZIRI DKT.NDUMBARO ARUHUSU KUSAFIRISHWA KWA TANI 1,683 ZA GUNDI KWENDA NCHI ZA NJE

NA LUSUNGU HELELA-WMU

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameruhusu kusafirisha jumla ya kontena 93 ya gundi ( utomvu) ambayo ni sawa na tani 1683 iliyokuwa tayari imeshavunwa wakati akitoa tamko la kuzuia usafirishaji wa malighafi hiyo kwenda nchi za nje
Ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha mara baada ya kupokea ushauri kutoka kwa Kamati ya Kumshauri Waziri kuhusu masuala ya misitu kabla ya kufanya mkutano wa Wadau wa mazao ya misitu kuwa gundi hiyo ambayo imekwisha vunwa inapozidi kukaa inapoteza ubora wake na hivyo kutokufaa tena kwa matumizi tena.

Dkt.Ndumbaro amesema, amelazimika kuruhusu kusafirishwa kwa tani hizo ili gundi hiyo isiweze kuharibika pamoja na kuepusha hasara ambayo ingewapata kwa wamiliki pamoja na serikali kukosa mapato kwani Serikali inapata mapato pindi malighafi hiyo inaposafirishwa.

"Hii gundi ni 'Chemicals' inavyozidi kukaa inabadilika rangi na Wataalamu wamenambia kuwa ikiendelea tu kukaa muda wake unaisha wa matumizi,"amesisitiza Dkt.Ndumbaro.

Gundi ni aina ya utomvu unaogemwa kwenye miti ya kupandwa aina ya misindano ambapo malighafi hiyo husafirishwa kwenda nchi za nje lakini hata hivyo hadi hivi sasa matumizi yake bado hayajaweza kufahamika kuwa inatumikwa kwa ajili ya kutengenezea vitu gani.

Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la kusitishwa kuvunwa na kusafirishwa kwa malighafi hiyo kwenda nchi za nje alilolitoa Dkt. Ndumbaro mwezi Oktoba akiwa mkoani Iringa mara baada ya kushindwa kupata maelezo ya kutosha kuhusiana na biashra ya bei ya gundi hiyo pamoja na matumizi yake huko inakosafirishwa nchi za nje hususani China.

Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameendelea kushikilia msimamo wake wa kusitisha zoezi la kuvuna utomvu huo hadi pale Chuo cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania ( TAFORI) zitakapotoa utafiti wake ambao kwa sasa bado haujakamilika juu ya athari ya miti inayovunwa gundi hiyo.

Akifafanua katazo hilo, Dkt.Ndumbaro amesema katazo hilo lina manufaa makubwa kwa Watanzania kwa ajili ya kutengeza ajira nyingi kwa wananchi

''Mara baada ya kukamilika kwa ripoti kutoka TAFORI na SUA na kujiridhisha kuwa uvunaji hauna madhara wafanyabiashara mtatakiwa kujenga viwanda hapa nchini na sio habari ya kusafirisha,'' amesisitiza Dkt. Ndumbaro.

Akizungumzia kuhusiana na Biashara ya Veneer, Dkt. Ndumbaro amewaeleza Wafanyabiashara hao kuwa yeyote atakayetaka kusafirisha lazima afuate masharti aliyoyato mwezi Noemba akiwa Jijini Dar es Salaam huku akiwata raia wa China wanaofanya biashara hiyo kupitia Chama cha Wafanyabiashara wa China kilichopo nchini kama Wadhamini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news