Waziri na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wanachapa kazi inayoendana na kasi ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan-Kasiana Mwanyika

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa,Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na wasaidizi wao katika wizara ili kuhakikisha Watumishi wa Umma wanaofanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu na uzalendo kwa taifa lao wanapewa vipaumbele vingi.
"Pale ambapo tutabaini kuna mtumishi mzembe, mla rushwa na mbadhirifu wa mali za umma sitokuwa tayari kumtetea lakini nitakuwa tayari kupambana na kumtetea mtumishi yeyote mwadilifu, mchapakazi na mzalendo kwa taifa lake muda wote asubuhi, mchana, jioni na usiku,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza hivi karbuni akiwa ziarani mkoani Kigoma.

Post a Comment

0 Comments