Wezi wa vyuma chakavu katika miundombinu ya barabara,alama wakalia kuti kavu, DC Nawanda afunguka

NA LUCAS RAPHAEL

MKUU wa Wilaya ya Tabora Mjini,Dkt. Yahaya Nawanda amewataka watu wanaojihusisha na wizi wa miundombinu na alama za barabarani waache kujihusisha na wizi huo kwani serikali itachukua hatua kali dhidi yao.
Vyuma chakavu.

Hatua hiyo ya mkuu wa wilaya imekuja hasa baada ya alama za barabarani kwa baadhi ya maeneo kadhaa kungolewa na kuibwa.

Akizungumza na DIRAMAKINI BLOG ofisini kwake,Dkt.Nawanda amesema,wananchi wanapaswa kuwa na uchungu na uharibifu na wizi unaofanyika kwani Serikali inatoa na kutumia fedha nyingi kutengeneza barabara hizo.

Amesema, wananchi ni lazima wawe na uzalendo wa nchi na mali zao, hivyo barabara hizi ni kodi zao kufanya hujuma na wizi ni jambo ambalo halitavumilika na atakayebainika atachukukuliwa hatua kali kwani atahesabika kama muhujumu uchumi wa nchi.
Mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa, barabara hizi ni mali ya wananchi wenyewe hivyo jamii kwa ujumla inatakiwa kuwa na uzalendo na uchungu dhidi ya uharibifu huo unaofanyika.

Dkt.Nawanda aliwataka pia wale wote wanaijihusisha na kufanya biashara ya ununuaji wa alama za baraarabni kuacha mara moja hujuma, kwani serikali itapoawabaini haitasita kwachukulia hatua kali.

“Nawataka na kuwasihi wanaofanya biashara ya vyuma chakavu wasiingie kwenye mtego wa baadhi ya wanaoharibu alama za barabarani na kuwauzia serikali itawakamata na kuwapeleka mahamakani,"amesema Dkt.Nawanda.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa polisi ama vyombo vya usalama pale wanapobaini wizi pamoja na watu wanajihusisha na hujuma hizo ili sheria ichukue mkondo wake.

Amesema kuwa, watu wanaofanya wizi na uharibifu wa miuondombinu ya barabara wanaishi na jamii inayowazunguka kwa ujumla na wanafahamika hivyo ni muda sasa wananchi wanapaswa kuwataja na kuwafichua ili serikali iwashughulikie kwa ukamilifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news