Ahmed Ally amrithi Haji Manara nafasi ya usemaji Simba SC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MTANGAZAJI wa AZAM TV, Ahmed Ally leo Januari 3,2022 ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano (Afisa Habari) katika Klabu ya Simba SC.
Hatua hiyo inafikiwa baada ya uongozi wa Simba kuachana na Msemaji wake, Haji Manara siku ya Julai 28, 2021.

Baadaye nafasi ya Manara ilizibwa na mwanahabari, Ezekiel Kamwaga ambaye alikaimu kwa miezi miwili.
Kupitia ukurasa wa Facebook wa Simba SC wameandika, "Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.

"Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano,"wameeleza

Kwa sasa, aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo,Haji Manara alijiunga na Yanga SC ambao wawili hao ni watani wa jadi enzi na enzi. 

Post a Comment

0 Comments