Azam FC yapeleka kilio kwa Yosso Boys FC, walala na mabao 5-1

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WENYEJI Yosso Boys FC wamejuta kukutana na Azam FC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 5-1.
Yosso Boys FC wamekubali kichapo hicho Januari 8,2022 katika Dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Ushindi wa Azam FC umenogeshwa na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo aliyetupia mawili dakika ya 40 kwa penalti na 66.
Huku beki Mghana, Daniel Amoah dakika ya 51 akitupia la tatu na kiungo, Ismail Aziz Kada dakika ya 57 na Munzil Abdallah aliyejifunga dakika ya 74.

Yosso Boys walifutwa machozi na Daudi Francis Hiluka dakika ya 19 ya mtanange huo.

Azam FC imemaliza na alama tisa kileleni mwa Kundi A ambapo washindi wa Kundi B na mabingwa watetezi, Yanga SC watakutana nusu fainali.
Aidha,washindi wa pili wa Kundi A, Namungo FC watacheza na washindi wa Kundi C, Simba SC.

Mitanange hiyo itapigwa Januari 10,2022 huku fainali ya Kombe la Mapinduzi ikitarajiwa kupigwa Januari 13,2022 katika dimba hilo la Amaan jijini Zanzibar.

Januari 7,2022 klabu ya Simba ilifanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi licha ya sare ya 0-0 na wenyeji, Mlandege FC.

Ni kupitia mtanange uliopigwa katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Simba ilimaliza kileleni mwa Kundi C kwa alama zake nne, mbili zaidi ya Mlandege.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news