Benki Kuu ya Tanzania yashiriki kwa ufanisi Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria 2022

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BENKI Kuu ya Tanzania imeshiriki Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria mwaka 2022 kuanzia Viwanja vya Mahakama Kuu Dodoma mpaka Viwanja vya Nyerere Square. 
Matembezi hayo ya leo Januari 23,2021 yameongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Baada ya matembezi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amezindua Maadhimisho ya Wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Uzinduzi ambao umekwenda sambamba na uzinduzi wa Nembo pamoja na Bendera ya Mahakama.

Mheshimiwa Rais ameeleza kwamba, kwa lugha nyingine sheria na taratibu za Mahakama zilizopo lazima ziendane na mipango iliyopo ya Serikali yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi kupitia Uchumi wa Buluu.
"Mimi binafsi nitafurahi sana kama wanasheria kutoka pande zote mbili za Muungano, mtakuwa na mijadala ya dhati kuhusu kwa kiasi gani, sheria na taratibu za kimahakama zinavyoweza kuboresha kwa lengo la kufanikisha dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ya ujenzi wa Uchumi wa Buluu,"amesema Rais Dkt. Mwinyi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amerejea kauli yake aliyoitoa Novemba 11,2020 katika hotuba ya uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pale aliposema kwamba Wazanzibari hawana budi kuigeuza bahari kuwa ndio shamba lao, kwani huko ndiko fursa za ajira za Zanzibar mpya zilizopo ambapo pia, huo ndio msingi wa dhana nzima ya Uchumi wa Buluu.
Amesisitiza kwamba, Zanzibar haikujaaliwa ardhi kubwa kwani ni nchi ya visiwa ambapo idadi ya watu wake imeongezeka mara tano katika kipindi cha miaka 56 ambapo mwaka 1964 Wazanzibari walikuwa laki 3 tu ambapo hivi sasa wapo takribani milioni 1.6. 

Katika hotuba hiyo Rais Dkt. Mwinyi alitoa wito kwa Wanasheria na wataalamu wa sheria, viongozi wa Mahakama na watumishi wa sekta za sheria kuielewa na kuifanyia kazi mipango mikuu ya uchumi wa Tanzania na kuwa huru kutoa ushauri wa kisheria Serikalini kwa lengo la kuifanikisha.
Rais Dkt. Mwinyi alisema kuwa Serikali zote mbili zinatambua kwamba zipo sheria ambazo huenda zikawa ni kikwazo cha kufikia matarajio ya kiuchumi na ustawi wa jamii ambapo sheria hizo zinahitaji kufanyiwa mabadiliko ili zifanikishe mipango ya uchumi wa kisasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news