CUF yaonyesha matumaini makubwa kutoka kwa Rais Samia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKURUGENZI wa Habari Uenezi na Mahusiano ya Umma wa Chama cha Wananchi (CUF),Mhandisi Mohamed Mshamu Ngulangwa ameanza mwaka mpya kwa kuongea na wana chama wa chama CUF wa tawi la Nia moja Kata ya Kiburugwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mhandisi Ngulangwa amewapongeza Wana CUF wa Nia moja kuanza mwaka wa 2022 kwa shughuli za chama.

Mhandisi Mohamed Ngulangwa baada ya kuwatakia kheri ya mwaka mpya 2022 aliwaambia mwaka 2021 ulikuwa mwaka wa misukosuko na majonzi nyanja zote.

"Tuliutumia sana kuomba na kujipa moyo kwa kukata tamaa kutokana na mauzauza mengi yaliyotokea. 2022 tunauanza kwa matumaini mapya,tukiwa na rais mpya mwenye nia ya kuwaweka watanzania pamoja ili kumalizia mchakato wa katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi,uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara,usawa na haki katika kila sekta,tunamuombea Mheshimiwa Rais,mama yetu, Mwenyezi Mungu amjaalie aweze kutembea kwenye maneno na dhamira yake,"amesema.

Post a Comment

0 Comments