IGP Sirro awavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123 waliotunukiwa nishani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Samia Suluhu Hassan.
Tukio hilo limefanyika leo Januari 21,2022 katika Makao Makuu ya Polisi mkoani Dodoma ambapo Mkuu wa Jeshi la Polisi amepewa madaraka hayo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama chini ya kifungu cha Sheria ya shughuli za Rais.

Akisoma taarifa ya kuvisha nishani hizo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Mihayo Msikhela amesema kuwa,Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa mamlaka hayo ametunuku nishani ya miaka 60 ya Uhuru, nishani ya utumishi uliotukuka na nishani ya utumishi mrefu na tabia njema.
Idadi ya Nishani zilizotunukiwa; Nishani ya miaka 60 ya Uhuru (5) ,Nishani ya Utumishi uliotukuka (58) na Nishani ya Utumishi mrefu na tabia njema (60).

Nishani ya miaka 60 imetunukiwa kwa majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo imetolewa kwa Maafisa na Askatri wa Jeshi la Wananchi Tanzania ,Maafisa ,Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza.

Hata hivyo ,kwa mujibu wa taarifa hiyo mapendekezo ya Nishani yaliyopokelewa ,kufanyiwa kazi na kuwakilishwa kwenye Kamati ya Nishani ya Taifa ni Nishani ya miaka 60 ya Uhuru 5,Nishani ya Utumishi uliotukuka (60),Nishani ya Utumishi Mrefu 53,Nishani ya Utumishi mrefu na Tabia njema 575 na Nishati ya Mwenge wa Uhuru 42,956.
Desemba 9, mwaka 2021,Rais Samia alitunuku Nishani kwa watumishi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama 893 katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments