Januari 11 ya majonzi kwa waandishi wa habari Tanzania

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mwanza (MPC) umewatambua waandishi wa habari waliofariki katika ajali.

Hayo yamesemwa na Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa klabu hiyo muda mfupi wakati akizungumza na waandishi leo Januari 11,2022.

"Ndugu waandishi wa habari na wadau wa habari, asubuhi ya leo tuliwataarifu taarifa ya awali juu ya ajali ya waandishi wenzetu wa Mkoa wa Mwanza.

"Baada ya kufika kwenye Zahanati ya Busenga nilipewa jukumu la kuwataambua marehemu.

"Waliofariki ni Husna Milanzi wa ITV,Johari Shani wa Uhuru Digital,Antony Chuwa ambaye ni Freelancer,Abel Ngapenda ambaye ni Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na Steven Msengi ambaye ni Afisa Habari Ukerewe.

"Majeruhi ni Tunu Heman ambaye ni Freelancer na Vany Charles kutoka Icon TV.

"Kwa sasa tupo njiani na miili ya wapendwa wetu kuelekea hospitali ya Mkoa ya Seketoure Mwanza,"amesema Soko.

Amesema,kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa magari yote mawili na amethibitisha vifo hivyo.

"Taarifa nyingine za uratibu kuhusu msiba tutawajuza.Mwanza Press Club tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu.Kazi ya Bwana haina makosa, jina lake lihidimiwe,"ameeleza Soko.

Ajali hiyo imehusisha magari mawili likiwemo la abiria aina ya Toyota Hiace na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara baada ya kugongana uso kwa uso leo Janauri 11, 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Bw. Emmanuel Luponya Sherembi, ameahirisha ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news