Karatu yatumia Bilioni 1.2/- kujenga madarasa 60

NA SOPHIA FUNDI

MPANGO wa Maendeleo kwa Ustawi na Mapambano Dhidi ya Uviko-19 umefanikisha ujenzi wa vyumba 60 vya madarasa katika Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.
Pichani ni mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba wakati akizindua madarasa yaliyojengwa kwa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa mapambano dhidi ya Uviko-19.

Akisoma taarifa kwa mkuu wa wilaya hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,  Karia Magaro wakati wa kukabidhi madarasa hayo amesema kuwa, ujenzi huo uligharimu kiasi cha sh.bilioni1.2 ambapo madarasa 58 yalijengwa katika shule za sekondari na madarasa mawili yalijengwa katika shule mbili shikizi.
Magaro amesema kuwa, madarasa hayo yamekamilika ikiwemo na samani zake na kufanya wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza masomo yao Januari bila kubughudhiwa kama ilivyokuwa zamani wazazi kuchangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na samani zake.

"Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, kwani wananchi wangekuwa wakichangishwa fedha kwa ajili ya miradi ya shule ikiwemo madawati na ujenzi wa madarasa,"amesema Magaro.
Amewapongeza wakuu wa shule pamoja na bodi zake kwa kushirikiana na wananchi hadi kukamilika ujenzi wa madarasa hayo ambapo alimtaka mkurugenzi kuona ni kwa namna gani wanaweza kupongeza shule tano zilizofanya vizuri katika ukamilishaji wa madarasa hayo.

Post a Comment

0 Comments