🔴 LIVE:Yanga SC vs Azam FC nusu fainali Kombe la Mapinduzi

MABINGWA watetezi wa taji hilo ambao ni Yanga SC wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam wanamenyana na Azam FC ambao pia ni wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam leo Januari 10, 2022 katika dimba la Amaan jijini Zanzibar.
Aidha, mchezo mwingine ni ule wa pili ambao utazikutanisha Simba SC wenyeji wa Jiji la Dar es Salaam dhidi ya Namungo FC ambao ni wenyeji wa Mkoa wa Lindi kuanzia saa 2:15 usiku.

Washindi kwenye mechi hizi watakutana kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Januari 13,2022 katika dimba hilo jijini Zanzibar.

Pia timu zote ambazo zinacheza leo ni zile zinazotoka Bara baada ya zile za Visiwani kuweza kuondolewa kwenye hatua ya makundi.

Post a Comment

0 Comments