Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar atoa rai kwa waumini kuhusu malezi

NA MWANDISHI MAALUM

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, amewakumbusha waumini wa dini ya Kiislamu nchini kujitahidi kuendeleza malezi mema ili kusaidia kupata viongozi bora nchini.
Mhe. Othman amayesema hayo Januari 7,2022 mara baada ya kukamilika kwa ibada ya  sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa Mahonda Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alhaj amesema, jamii inakabiliwa na changamoto kubwa ya malezi kwa vijana kukosa maadili na kusisitiza kwamba ni vyema kwa waumini kuitumia vizuri neema ya vizazi vinavyopatikana kwa kila mmoja kutimiza wajibu katika kuendeleza malezi mema yanayozingatia misingi na maadili bora ya dini ya Kiislamu.

Alisema kwamba, binadamu wamepewa daraja kubwa kutokana na kuomba kupata watoto wanaoweza kuandaliwa kuwa viongozi na wafuasi wema na kuepusha matatizo makubwa yanayoweza kusababishwa na vijana kukosa malezi na maadili kwa mujibu wa miongozo ya Uislamu.

Aidha, Alhaj Othman ameikumbusha jamii ya Zanzibar kutambua kwamba neema ya kizazi aliyoileta Mwenyezi Mungu hapana budi kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuwalea vyema kwa kuzingatia maadili ili taifa liweze kuwa na vijana wema wenye maadili yatakayosaidia na kuchangia maendeleo ya taifa.

Mapema Katibu wa sala ya Ijumaa katika Msikiti huo Sheikh Salim Gharib, alikumbusha waumini na viongozi umuhimu kumcha Mwewnyezi Mungu na kutenda haki wanapotekeleza majukumu, wajibu na shughuli zao mbalimbali wanazopewa pamoja na kuchunga haki kwa mujibu miongozo ya dini na taratibu nyingine mbalimbali zilizopo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news