Mhandisi Hhayuma arejesha fomu mchakato wa kumrithi Ndugai nafasi ya Spika

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBUNGE Jimbo la Hanang' mkoani Manyara, Mhandisi Samwel Hhayuma amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhandisi Hhayuma amerejesha fomu hiyo leo Januari 15, 2022 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Amesema, kujitokeza kwa watu wengi katika hatua ya kuomba ridhaa ya chama kuchaguliwa kuwa Spika ni hatua nzuri kwani kuwa na chaguzi nyingi inakuwa inatoa nafasi kupata mtu sahihi.

“Mimi ni mbunge wa Jimbo la Hanang', wana Hanang' wameniamini, nikipata nafasi ya kuongoza Mhimili wa Bunge maana yake nitwaongoza wabunge wenzangu, ninavyo vigezo vyote vya kuwaongoza, nimekuwa kiongozi toka nikiwa mdogo, hekima na busara za kuongoza ninazo, mimi najiona Kiongozi,"amesema.

Aidha,wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muunga wa Tanzania hadi Januari 14, walikuwa wamefikia 66. 

Idadi hiyo ilitangazwa na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomoni Itunda mbele ya vyombo vya habari katika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news