Msanii wa Bongo Fleva Baba Levo atunukiwa udaktari wa heshima

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MSANII wa Bongo Fleva nchini na aliyewahi kuwa Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu Baba Levo ametunukiwa udaktari wa heshima.
Udaktari huo ametunukiwa na College of Health and Allied Sciences cha jijini Mwanza ambapo cheti chake kinabainisha kuwa, heshima hiyo imejikita katika afya,siasa,sanaa na burudani.

Msanii huyo ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi FC ameyabainisha hayo kupitia cheti alichoambatanisha katika ukurasa wake wa kijamii.
"JANA UONGOZI WA CHUO CHA MADAKTARI City College ULINIPATIA CHETI CHA DAKTARI WA HESHIMA...!!! #PHD YA #AFYA #SIASA #SANAA NA #BURUDANI 😭😭😭 NISEME NASHUKURU SANA KWA HESHIMA WALIYO NIPATIA..!!🙏🙏🙏🙏🙏 FROM NOW CALL ME DOCTA..!!🙏🙏🙏'',"ameeleza Baba Levo.

Post a Comment

0 Comments