Mtumishi wa Umma amshukuru Mungu kwa Taifa kumpata Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mchengerwa na Naibu Waziri Ndejembi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeendelea kupongezwa kila kona huku watumishi wakiendelea kumshukuru Mungu kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya watumishi na kuwaletea maendeleo Watanzania.
Vilevile,wanamshukuru Mungu kwa kumpa Rais wasaidizi wachapa kazi akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na bidii kwa watumishi wa umma nchini ili kuwezesha mipango ya Serikali katika nyanja mbalimbali kufikiwa kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments