Mwalimu mstaafu Bi.Wambi Mwanyanje amshukuru Katibu Mkuu-UTUMISHI Dkt.Laurean Ndumbaro kwa kumuelekeza mwajiri kumrejeshea cheo chake

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAFANIKIO haya yanakuja ikiwa hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika uongozi wake hatowasaliti katika kutetea stahiki zao Watumishi wa Umma wanaofanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu na uzalendo kwa taifa lao.
Akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Mchengerwa amesema atahakikisha anasimamia haki na stahiki za Watumishi wa Umma nchini kwa lengo la kuwaongezea morali ya utendaji kazi kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita imekusudia.

Kufuatia uamuzi wake wa kusimamia haki na stahiki za Watumishi wa Umma, Mhe. Mchengerwa ametoa rai kwa watumishi wote wa umma nchini kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan badala ya kufanya kazi kwa mazoea kwani wasipowajibika hatokuwa tayari kutetea stahiki zao.

Post a Comment

0 Comments