Mwanasheria Mkuu wa Serikali aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali SADC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TANZANIA imeungana na nchi nyingine Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali uliofanyika leo Januari 25, 2022 kwa njia video. 

Mkutano huo umejadili kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria sambamba na kufanya tathimini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo na itifaki mbalimbali za jumuiya. Miongoni mwa ajenda zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na; majadiliano ya Ushauri wa Kisheria kuhusu Kufanya Mikutano ya Double Troika, majadiliano ya Ushauri wa kisheria kuhusu Mapitio ya Hadidu za Rejea za Kamati ya Mabalozi na Makamishna Wakuu wa SADC walioidhinishwa na Jumuiya hiyo, kupitia na kufanya Marekebisho ya Mkataba wa Mahakama ya Utawala ya SADC, kujadili Rasimu ya Mkataba wa Marekebisho ya Itifaki ya Maendeleo ya Utalii katika SADC na kujadili Mkataba wa Makubaliano ya Nchi Wanachama wa SADC kuhusu uanzishwaji wa Kituo cha Operesheni za Kibinadamu na Dharura cha Jumuiya.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umeongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Jaji Dkt.Eliezer Mbuki Feleshi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news