Naibu Waziri Ummy Nderiananga awasili Pemba, azindua kisima cha maji safi na salama

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Ummy Nderiananga amezindua kisima cha maji safi na salama katika shule ya msingi inayohudumia watoto wenye mahitaji maalum ya Mchanga Mdogo iliyopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akimtwika ndoo ya maji mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mchanga Mdogo Pemba mara baada ya kuzindua rasmi kisima cha maji kinachotarajiwa kutatua changamoto za maji shuleni hapo Januari 4, 2022.

Naibu Waziri huyu amezindua ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi Visiwani humo iliyolenga kutembelea na kujionea shughuli za utekelezaji za masuala ya watu wenye ulemavu Pemba tarehe 04, Januari, 2022.

Akiwa amaeambatana na Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Hamad Chande alieleza furaha yake ya uchimbaji wa kisima hicho kitakachosaidia kutatua changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama shuleni hapo huku akishukuru wafadhili waleta huduma hiyo.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akifurahia jambo na mwanafunzi mwenye ulemavu, Fatma Hamis anayesoma shule ya Msingi ya Mchanga Mdogo iliyopo Wilaya ya Wete Pemba, mara baada ya kuzindua kisima cha maji shuleni hapo.

“Kipekee niwapongeze Taasisi ya Rehema Foundation na Ofisi ya Mbunge wa Kojani kwa kuchimba kisima na kuonesha umuhimu wa kuleta huduma hii muhimu hasa kwa kundi letu la wenye ulemavu hatua itayosaidia kuboresha mazingira yao na kuchangia ufaulu wao,hii napongeza sana,” alisema Mhe. Ummy.

Naye Mbunge huyo wa Kojani ambaye pia ni Naibu waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, aliyaeleza furaha yake ya kukamilika kwa maono hayo huku akisema itasaidia kuchagiza utulivu na kusoma kwa bidii.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akifurahia jambo na mwanafunzi mwenye ulemavu, Fatma Hamis anayesoma shule ya Msingi ya Mchanga Mdogo iliyopo Wilaya ya Wete Pemba, mara baada ya kuzindua kisima cha maji shuleni hapo.

“Niwapongeza naibu waziri kuona umuhimu wa kujumuika na jamii yetu na kuzindua kisima hiki, na kisima hiki ni miongoni mwa visima vitano tulivyoomba Rehema Foundation kuchimba na wameshachimba vinne na leo wamehitimisha cha tano, tunawapongeza,”alisema Mbunge.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu)Mhe. Ummy Nderiananga akizumza na mwanafunzi mahitaji maalum, Fatma Hamis anayesoma shule ya Msingi ya Mchanga Mdogo iliyopo Wilaya ya Wete Pemba, mara baada ya kuzindua kisima cha maji shuleni hapo.

Kwa upande wake mwakilishi wa taasisi ya rehema Foundation Bw. Mohamed Assa alieleza kuwa, wataendelea kusaidia huduma za kijamii kwa wakazi wa Pemba ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuunga mkono jitihada za serikali na kuwaasa kukitunza ili malengo ya uwepo wa kisima hicho yatimizwe.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima cha maji pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Chande yenye kuhudumia wanafunzi wenye ulemavu iliyopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Kisima hicho kimefadhiliwa na Rehema Foundation kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge huyo.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw.Suleiman Kombo alishukuru jitihada za taasisi na ofisi ya Mbunge huku akiwaasa wanafunzi na wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha miradi kama hiyo inalindwa na kutunzwa kwani inasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa jamii kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments