Ndugai:Nimejiuzulu Uspika kwa hiari yangu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu nafasi hiyo leo Januari 6, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa yake kwa umma, Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kujiuzulu nafasi hiyo ikibainisha kuwa uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa umma wa watanzania kuwa leo tarehe 6 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania.
“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria nyingine,” amesema Ndugai kwenye taarifa yake kwa umma.

Post a Comment

0 Comments