PBZ BANK yaweka kambi viwanja vya Maisara

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ BANK) imeweka kambi katika viwanja vya Maisara jijini Zanzibar kushiriki Maonesho ya Nane ya Biashara kama sehemu ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa benki hiyo, huduma wanazotoa viwanjani hapo ni pamoja na ufunguaji wa akaunti, fursa za mikopo, kutoa na kuweka pesa.

Sambamba na kuunganishiwa huduma za mobile banking, kupata kadi ya VISA, utatuzi wa changamoto kuhusiana na huduma zao ikiwemo ushauri juu ya masuala ya kifedha kwa ujumla wake.
"Tutakuwepo kuanzia leo Januari 2, 2022 hadi Januari 15,2022.Karibuni wote PBZ BANK, BENKI YA WATU,CHAGUO LA WATU,"imeeleza benki hiyo.

Post a Comment

0 Comments