Pongezi Maalum kwa Mheshimiwa Mhagama, WN ORMUUUB, Naibu Waziri Mheshimiwa Ndejembi, Dkt.Ndumbaro, Katibu Mkuu na Bw.Daudi, Naibu Katibu Mkuu

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC), Bw. Mathew M. Kirama amewapongeza Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR MUUUB), Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb), Naibu Waziri (OR MUUUB), Dkt. Laurean J.P. Ndumbaro, Katibu Mkuu (OR MUUUB) na Bw. Xavier M. Daudi, Naibu Katibu Mkuu, (OR MUUUB) kwa kuaminiwa kwao na kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katibu wa Tume, Bw. Mathew M. Kirama amesema kupitia salamu za pongezi alizozituma kwao kuwa Menejimenti na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma wanawaahidi ushirikiano na kuchapa kazi, "KAZI IENDELEE".
Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298. (Pamoja na marekebisho ya mwaka 2019).

Post a Comment

0 Comments