Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo Januari 7,2022

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Januari 7,2022 amefanya uteuzi.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Jaji Aziza Idd Sued kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 7,2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza leo Januari 7,2022.

Post a Comment

0 Comments