Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika mazishi ya aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji ZIPA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na waumini wa Kiislam katika sala ya kusalia jeneza la marehemu Salum Khamis Nassor, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Rais Mstaafu wa Zanzibar, Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Alhaj Balozi Seif Ali Iddi wakijianda kubeba jeneza kwa ajili ya ibada ya kusalia mwili wa marehemu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea Marehemu Salum Khamis Nassor, ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Rais Mstaafu wa Zanzibar, Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Alhaj Balozi Seif Ali Iddi na kulia kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kumpa mkono wa pole Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein kushoto kwa Rais baada ya kumalizika kwa Ibada ya kusalia jeneza la Marehemu Salum Khamis Nassor, aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji ZIPA,Ibada hiyo iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar leo 22-1-2022.(Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news