Rais Dkt.Mwinyi atoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Ramadhan Hamza Chande,Fatma Suleiman

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Ramadhan Hamza Chande, Mwakilishi mstaafu wa Jimbo la Jang'ombe liliopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi alitumia fursa hiyo pia kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Bi Fatma Suleiman, Diwani mstaafu wa Kwaalinato, Jimbo la Jang'ombe, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuzisihi familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu awalaze marehemu wote mahali pema peponi, Amin.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments