Rais Dkt.Mwinyi awalilia waliofariki katika ajali wakiwemo waandishi, atuma salamu za pole kwa Waziri Nape Nnauye

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemtumia salamu za pole Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknonojia ya Habari, Nape Nnauye kufuatia ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Busega mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu wakiwemo waandishi wa habari.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa salamu hizo za pole kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa habari.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuwasihi ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa habari kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, Amin.

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu kuwaponya kwa haraka wale wote waliopata majeraha kutokana na ajali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news