Rais Samia afanya uteuzi mwingine muda huu

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Januari 8,2022 amemteua, Bw.Willy L.Machumu kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Machumu alikuwa Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi.

Aidha,anachukua nafasi ya Dkt.Seif A.Shekalaghe aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya.Post a Comment

0 Comments